Kiswahili

Karibuni jamani kwenye kikundi kwa wanaotaka kujifunza Kiswahili. Mtu yeyote anayetaka kujifunza, karibu sana.

Labda nianze kwa kujitambulisha. Kwa jina, ninaitwa Nicholas. Sasa niko chuoni nchini Marekani, ila nilijifunza Kiswahili nchini Tanzania. Ninaipenda lugha ya Kiswahili, ndiyo maana nikaanzisha kikundi hiki. Hata kama umeanza kujifunza hivi karibuni, ama uwezo wako wa kuongea bado ni mdogo, ningependa kuanza kuzungumza nawe ili tuweze kusaidiana.